MAELEZO YA AWALI

KUHUSU CHUO

  1. Chuo kimeanzishwa kwa lengo la kupambana na umaskini. Kutoa elimu bora yenye hadhi ya kimataifa ili kumwezesha msomaji kujiajiri au kuajiriwa na kuondokana na umaskini.
  2. Kujenga usawa kati ya wenye nacho na wasio nacho kwa kutoa elimu bora inayozingatia mabadiliko ya sayansi na teknologia.
  3. Kujenga wanafunzi uwezo wa kukabiliana na mazingira ya kitanzania kwa kuweza kubadilisha taaluma walio nayo kuwa ajira kwa ustawi mpana wa wa Taifa

SIFA STAHIKI

  1. Awe na ufaulu unaotakiwa.
  2. Awe amesitisha masomo katika chuo kinachotambulika na NACTE
  3. Awe anatoka maeneo ya kijijini
  4. Awe ana mwamini Mungu,kumpenda na kumtumikia
  5. Awe tayari kufanya kazi zote za chuo

WAJIBU WA MFADHILIWA.

  1. Kusoma kwa bidii (kudorora kwa masomo kutasimamisha ufadhili)
  2. Kujitoa kwa ajili ya wengine. Kumcha Mungu na kufanya kazi kwa bidii.
  3. Kufanya kazi mbalimbali kwa Kuzingatia miongozo ya chuo.

JINSI YA KUOMBA UFADHILI.

Maombi yatafanyika kwa Kujaza fomu maalumu ya ufadhili inayopatikana chuoni au bonyeza kitufe hapo chini kufanya maombi Online

FOMU YA MAOMBI YA UFADHILI

2026/2027 Academic Year

i. Ikiwa utachagua kategoria D au E lazima ukae kwenye hostel za chuo na uwe na uwezo wa kuchangia 250,000 za hostel kwa mwaka.
ii. Ufadhili hauhusishi gharama za Field na bima ya afya. Mnufaika wa ufadhili sharti uwe na uwezo wa kuchangia gharama hizo.
iii.Ukiwa mnufaika una changamoto yoyote unapaswa kuwasiliana na ofisi ya ufadhili.
iv. Mnufaika atajigharamia gharama ya chakula yeye mwenyewe.
Nakubaliana na vigezo na masharti ya ufadhili huu. *

ADA YA MAOMBI YA UFADHILI

Ada ya maombi ya ufadhili ni kiasi cha Tsh elfu Thelathini (30,000). Fedha hii ilipwe kwenye account ya chuo.